Kwanini mwandishi afanye book cover makeover?
Fikiria una sekunde saba tu kumshawishi msomaji anunue kitabu chako ungefanya nini?. Katika kila utafiti unaofanyika kumwuliza msomaji nini kilimfanya akanunua kitabu fulani, asilimia kubwa husema jalada la kitabu lilikuwa na nafasi kubwa sana kumshawishi.
Jalada la kitabu lina nafasi ya pekee kufanya kitabu chako kiuzike ama kisiuzike. Ili kuendelea kuongeza mauzo ya kitabu chako, mwandishi anaweza kutumia mbinu ya kubadilisha muonekano wa jalada. Kubadilisha muonekano wa jalada la kitabu baada ya muda fulani huitwa book cover makeover.
Utafiti uliofanywa na mwandishi Derek Murphy ulionesha kuwa mwandishi anapobadilisha muonekano wa jalada la kitabu, mauzo yake huongezeka mara mpaka mara tatu. Huwezi kuwa na jalada la kitabu lile lile miaka nenda rudi, muda unafika inabidi ubadilishe kitabu kipate muonekano mpya.
Nimekuandalia sababu chache kwanini ni lazima kufanya book cover makeover kwa mwandishi wa vitabu, sababu hizo ni kama ifuatavyo;
1. Kuongeza mauzo ya kitabu. Hii ndiyo sababu kubwa zaidi. Unapofanya book cover makeover unapata muonekano bora zaidi kuliko wa mwanzo. Msomaji huvutwa na jalada la kitabu linaloonekana vizuri hivyo muonekano mpya na bora wa kitabu chako utaongeza mauzo ya kitabu chako.
2. Mabadiliko ya soko la vitabu. Soko la vitabu hubadilika na inapotokea hivyo unaweza badilisha muonekano wa jalada la kitabu ili kuendana na mabadiliko hayo. Unaandika kitabu ili uuze na kisomwe na wasomaji. Ladha ya wasomaji inapobadilisha soko la kitabu, basi nawe huna budi kufanya book cover makeover ili uweze kuwanasa na kitabu chako kiuzike.
3. Mwelekeo mpya wa muonekano wa jalada za vitabu. Hii ni sababu nyingine yaw ewe kufanya cover makeover. Jalada za vitabu huwa zina mwelekeo fulani. Ukilinganisha jalada za vitabu vya miaka ya 90’s na miaka ya leo utaona tofauti kubwa. Inapotokea mwelekeo wa jalada za vitabu zinabadilika, unaweza kubadilisha muonekano wa jalada la kitabu chako kuendana na mwelekeo huo.
Kwa ujumla wake book cover makeover inakupa nafasi ya kupata la jalada la kitabu litakalouza kitabu chako zaidi.
Je! Ni wakati sasa unataka kubadilisha muonekano wa jalada la kitabu chako? DL Bookstore tumekuwa tukiwasaidia waandishi wengi kupata muonekano mpya wa jalada za kitabu vyao, na tunataka kukusaidia na wewe upate huduma hii. Upo tayari? Bofya hapa chini,
Soma Makala zingine,
1. Mambo 3 ya kuzingatia kupata jina la kitabulinalouza sana.
2. Njia Nne Za Kumsaidia Muandishi Kuongeza OrodhaYa Imeli [Baruapepe) Za Wasomaji Wake.
3. Hatua tano za kuwatambua wasomaji wako walengwa.
Unataka kujua zaidi kuhusu uandishi wa vitabu? Soma kozi bure HAPA na kuwa wa kwanza kupata taarifa za kozi mpya kila inapowekwa.